MGOMBEA UBUNGE CHALINZE AJERUHIWA KWA MAPANGA.
MGOMBEA
Ubunge katika Jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,
Ramadhani Mgaya (pichani juu) kupitia chama cha AFP amejeruhiwa kwa
mapanga na watu wasio julikana.
Mgaya
amesema amevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye hamfahamu majira ya saa
sita za usiku akiwa katika nyumba ya kufikia wageni ya Goodtime
Chalinze.
"Nimevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye simfahamu ahsante uongozi wa Chadema kwa kunisaidia," alisema Mgaya.
Mgaya amesema ameumia mikononi wakati akipangua nakujitetea maana mvamizi alikuwa na panga.
Mbali
na yeye pia amesema kiongozi wa Chadema, Mwita Waitara naye alijeruhiwa
kwa kuwa alikuwa mmoja ya watu waliokuwa wakimsaidia.
HATAR
ReplyDelete