Mashujaa wa Tanzania watinga bungeni.
Timu
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto
wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye
fainali imetambulishwa jana (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu
la Katiba mjini Dodoma.
Baadaye timu hiyo ilipata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Saa 10 jioni ilitembeza kombe hilo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.
Jioni
iliandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini
Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS