Mafikizolo kutua Leo ndani ya Dar es Salaam.

Kundi kutoka Afrika Kusini Mafikizolo
linatarajia kuwasili leo kuja kwa lengo la kutoa burudani ya kutosha na
kufanya Tamasha kubwa pale Mlimani City Dar es Salaam hapo tarehe 5
April.
Ni Kundi linalounganisha vijana
wawili Nhlanhla Nciza, na Tebogo Madingoane ambao wanafanya vizuri na
kupendwa na watu wengi kwa staili ya mziki wao ‘Kwaito’ kupitia vituo
mbalimbali vya Radio na Television kwa nyimbo zao mbalimbali ikiwemo
Ndihamba Nawe,Nisixoshelani,Happness na Khona.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS