MTOTO WA MIAKA 14 AMUUA MUMEWE WIKI 1 BAADA YA NDOA.

Wasilu
Umar amemuua Mume wake ambae alikua na umri mara mbili ya umri wake kwa
kumuwekea sumu ya panya katika chakula chake kitendo kilichosababisha
watu wengine watatu kufariki na 10 kukimbizwa hospitali baada ya
kuhusika kwenye hicho chakula.
Baba
wa mtoto huyo alimlazimisha kuolewa na mwanamme huyo mwenye umri wa
miaka 35 ambapo harusi yao ilifanyika wiki iliyopita hukohuko kaskazini
mwa Nigeria ambako ni maarufu kwa kuoza watoto wakiwa na umri mdogo.
Polisi
wamekua wakijaribu kusitisha ndoa hizo za kulazimishwa ambapo baba wa
Mtoto anaweza kushtakiwa juu ya hilo kosa ila bado hivyo vitendo
vinaendelea.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS