Wema Sepetu na Aunt Ezekiel Wamwingiza JB Mkenge.
IMEKULA kwake! Wauza nyago kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu
na Aunt Ezekiel Grayson wamemuingiza mkenge staa mwenzao, kaka mkubwa
Jacob Steven ‘JB’ baada kukubali mwaliko kisha kumkatalia dakika za
mwisho.
Habari za ndani zilidadavua kwamba JB na wasanii hao walitakiwa kusafiri
kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa huko ambapo
walipelekwa na uongozi wa Ukumbi wa Princess Cassino uliopo Posta jijini
Dar.
Katika hali ya kushangaza, uongozi huo ukiwa tayari umeshawakatia tiketi
za daraja la kwanza (first class) zinazogharimu kama dola elfu moja
(zaidi ya Sh. milioni 1.6) kila mmoja na baadhi ya wasanii kama Vincent
Kigosi ‘Ray The Greatest’ na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Wema na Aunt
Ezekiel walikataa siku moja kabla ya safari.
Chanzo chetu makini kilipenyeza habari kuwa, Wema na Aunt walichomoa
safari hiyo baada ya kuhisi haikuwa na maslahi kwao na walivyopeleka
maombi yao ya kimaslahi kwa JB, aliwaambia ni safari ya kujifurahisha na
hakuna fedha yoyote watakayopata.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Aunt ambaye
alikiri kuchomoa safari hiyo baada ya kushindwana kimaslahi.
“Unajua ile ni kwenda kutangaza biashara ya mtu kwa hiyo sisi
tuliwatajia kiasi cha fedha ambacho tulikitaka kulipwa lakini
tulishindwana ndiyo maana tukakataa kusafiri maana hatuwezi kufanya kitu
ambacho hakina maslahi kwetu na kwenda kuwafaidisha wengine,”
alifunguka Aunt.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ aliilaani
safari hiyo na kusema kwamba JB ni mnafiki kwani aliwachagua wasanii
wachache kwa upendeleo ambao baadhi yao wamemwangusha kwa kutokwenda.
“Ukweli nimegundua JB ni mbinafsi, nilikuwa naambiwa lakini nikawa
namtetea, sasa nimeamini kwamba hafai akirudi lazima nitamuita,
nitazungumza naye kwa nini aliamua kufanya hivyo wakati kila kitu
kinapotokea iwe safari au vitu vingine huwa sisi Bongo Movie Unity
tunashirikishana lakini kwa hili ameona afanye mwenyewe,” alisema Steve
Nyerere.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS