MAMA WA MIAKA 50 AJIFUNGUA KWA NJIA YA KAWAIDA WATOTO WA AJABU HUKO HANDENI-TANGA
![]() |
Mwajuma Seif-Sio picha yake ya kipindi hiki |
Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake
walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya
upandikizaji.
Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa
kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa
katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka
rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake
wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia
ya upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika
umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.
Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia
mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni
mtoto wa ajabu aliyemzaa .
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya
Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa
na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na
tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi.
Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra
sound (kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo
yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga,
Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake.
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza kumsafirisha
kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi maalumu hadi siku ya
kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye
umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.
Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa hakuwa wa
kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji na saa moja
baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku moja na akafariki.
“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana. Huu ni
uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka maji hadi mwili
ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea kuishi kwa saa 24,”
anasema Dk Mushi.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili, lakini
iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa mbali. Hana
kiuno wala mikono.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS