VIJANA WAUZA JINA LA TANZANIA DUNIAN

Timu ya watoto wa Tanzania iliyonyakua kombe la dunia
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya nchi hiyo kwa kutwaa
Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Tanzania imesema Rais Kikwete afurahishwa jinsi watoto hao walivyonyakua kombe hilo la dunia.Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ilipangwa kundi la 2 ambapo pia zilikuwapo timu kutoka Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi.
Makundi yaliyopangwa yalikuwa matatu.
Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kumenyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwenye fainali kwa mabao 3-1.
"
Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi". Rais amesema na kuwaasa watoto "ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya" Ameongeza Rais Kikwete .