Translate

Friday, May 23, 2014

JAMANI TANZANIAA DA HATA SITO HAMA NAKUPENDA TANZANIA


Jozani Forest - Zanzibar
 Ukiwa unapenda wanyama pori basi hata kama utaenda visiwani utatamani uwaone hata kama ni wadogo na wachache. Visiwa vya Zanzibar, vimejaaliwa kuwa na aina ya pekee ya mbega ambao wanapatokana Visiwani humo tu. Hao ni Zanzibar Red colobus monkeys - Mbega wekundu wa Zanzibar. Na msitu wa Jozani ndio eneo mahususi lililotengwa kuwahifadhi na kuwapa fursa wengine kuja kuwaona viumbe hawa adimu. Tofauti na misitu na hifadhi nyingi za Hapa nchini, Msitu wa Jozani mgeni hutembea kwa miguu kuwasaka Mbega walipo. inategemea na muda na hali ya mazingira kwani unaweza tembea kwa masaa kadhaa ili kuwapata. Siku hii ilituchukua muda mfupi sana kuwaona kwani ilikuwa ni mida ya jioni na walikuwa wamesogea karibu kabisa na geti la kuingilia kwenye hifadhi.


POLISI mkoani Morogoro, inaendelea kuchunguza kilichotokea mpaka mtoto mkoani hapa, akateswa na mzazi mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, amesema, baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro alitakiwa kwenda kutoa maelezo kituoni jana  lakini hakutokea.
 
Kamanda Paul alisema jana kuwa, walimtafuta mzazi huyo kwa simu ili kumkumbusha umuhimu wa kufika Polisi kutoa maelezo, lakini simu zake zilikuwa zimezimwa.
 
Habari Leo  ilifika kwa mwajiri wake katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambako hakuwepo kwa kuwa aliaga kwamba amekwenda katika Kituo cha Ustawi wa Jamii, alikodai kuwa aliitwa.
 
Hata hivyo, mwandishi alipofika katika ofisi hiyo, lilihakikishiwa na  Ofisa Ustawi wa Jamii, Oswin Ngungamtitu, kuwa Mvungi hakuwa amefika katika eneo hilo, wala hakukuwa na mwito wa yeye kufika katika ofisi hiyo.
 
Katika tukio lingine la kutia shaka, Habari leo  lilipohojiana na Mvungi katika nyakati tofauti juzi, alitoa taarifa mbili tofauti, kuhusu sababu za kumuacha mwanaye kwa mama mkubwa wake, Mariam Said, aliyemuweka katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu.
 
Katika mahojiano ya awali, Mvungi alidai baada ya mzazi mwenzake, Mwasiti Ramadhan kufariki dunia, alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.
 
Alidai kwa kuwa alikuwa ameoa, alikubaliana na upande wa pili wa familia ya marehemu, kuwa mwanaye huyo alelewe na mama yake mkubwa, Mariamu.
 
Katika mahijiano na mwandishi mwingine juzi hiyo hiyo, Rashid alidai mwanae huyo alichukuliwa na Mama yake mkubwa ili kumlea akiwa na umri ndogo na mara zote alikuwa akipeleka fedha za matumizi.
 
Alidai kwa mara ya mwisho alimwona mwanae huyo miezi miwili iliyopita akiwa na afya ya kuridhisha, wakati taarifa zilizotolewa na Mariam, zilidai kuwa mtoto huyo hajaogeshwa tangu Julai mwaka jana.
 
“Kila nikienda kumwona nyumbani kwao sikubahatika kumwona , nilikuwa nikiambiwa amelala ama ametoka na watoto wezake...isipo kuwa miezi miwili iliyopita,” alidai Rashid kauli inayoonesha kuwa mtoto huyo alikuwa akitoka na wenzake wakati majirani walitoa ushahidi kuwa hawakuwahi kufahamu uwepo wa mtoto katika nyumba hiyo.
 
Taarifa kutoka katika Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, zimeeleza kuwa baada ya uchunguzi wa awali wa afya ya mtoto huyo, alibainika kuwa na niumonia, ulegevu wa viungo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mifupa katika mwili wake kuvunjika.
 
Daktari Mshauri wa watoto, Hores Msaky alipozungumza na Habari leo  jana, alisema walimpokea mtoto huyo juzi akiwa katika hali ya uchafu usio wa kawaida.
 
Msaky alisema waliamua kumfanyia vipimo vya awali pamoja na picha za X ray, wakagundua kuwa mifupa yake si ya kawaida, inaonekana imevunjika ingawa hawajajua nini kimemvunja.
 
“Tunachokifanya hivi sasa ni kujaribu kujua tatizo hilo limetokana na nini,” alisema daktari huyo .Hata hivyo Msaky alisema kuwa hospitali hiyo haina vifaa vingi vya kupimia mifupa, hivyo imeshauriwa apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi .
 
Muandishi wa habari hizi alifanikiwa kuingia wodi aliyolazwa mtoto huyo na kumkuta akiwa amechangamka, na alipoulizwa anaendeleaje alisema anasikia maumivu katika sehemu ya kifua .
 
Mtoto huyo alikuwa akidhulumiwa haki yake ya utu na kuteswa kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa kufungiwa ndani ya boksi kama mnyama, ili asiamumbukize mama mlezi virusi vinavyosababisha Ukimwi.
 
Unyama huo wa kusikitisha, ulikuwa ukifanyika muda wote huo kwa mtoto huyo Morogoro mjini katika mtaa wa Azimio bila kuripotiwa popote, huku wakazi na majirani wa nyumba hiyo wakisikia akikohoa na kulia usiku, na baba yake mzazi akiendelea na maisha kwa kumuogopa mkewe. Wakizungumza na gazeti hili juzi majirani hao walidai Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010, lakini hawakuwahi kumuona akiwa na mtoto.
 
Hata hivyo majirani hao walikiri kwamba walikuwa wakisikia mtoto akikohoa na kulia hasa nyakati za usiku, lakini walikuwa na wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga watu waliouawa kishirikina au kwa jina linguine misukule.
 
Hatimaye juzi mateso ya mtoto huyo yalipungua, baada ya msamaria mmoja kupata taarifa sahihi, kwamba ndani ya nyumba hiyo kuna kiumbe asiye na hatia aliye katika mateso na kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo.
 
Zongo akiwa katika kazi za kawaida katika mtaa huo, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kuna mwanamke, Mariamu Said, amemficha mtoto ndani ya boksi na hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
 
Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta mwenyeji wake, Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagalana na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo ambapo walimkuta mtuhumiwa, Mariamu na kuanza kumuhoji kuhusu tuhuma hizo.
 
Kwa mujibu wa Zongo, wakati mtuhumiwa akijibu maswali aliyoulizwa huku akibabaika, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa Mariamu kwa nguvu, hatua iliyomuokoa mtoto huyo kutoka katika mateso ya zaidi ya miaka mitatu.
 
Ofisa huyo na mwenyeji wake walimkuta mtoto huyo ametapakaa uchafu uliotokana na kinyesi na mkojo, kwa kuwa boksi hilo lilikuwa chumba chake cha kulala, meza yake ya chakula na maji na choo kwa ajili ya haja ndogo na kubwa.

List ya waigizaji matajiri duniani.

Screen Shot 2014-05-23 at 9.40.55 AMWapenzi wengi wa filamu duniani watakuwa wanalitambua jina lake ambapo kwa Tanzania ni maarufu zaidi uswahilini lakini duniani ndio anatajwa kuwa muigizaji anayejulikana zaidi.

Jina lake ni Shahrukh Khan ambae ni mwigizaji wa filamu kutoka India ambapo jana ametengeneza headlines baada ya kutajwa na jarida la maswala ya fedha la Wealth-X la Singapore ndio mwigizaji tajiri zaidi Asia pia anashika nafasi ya pili duniani nyuma ya comedian Jerry Seinfeld ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani milioni 820.
Jerry Seinfeld
Jerry Seinfeld
Khan ambaye ni maarufu kwa jina la Kingh Khan ana utajiri wa $600m akiwa kawazidi waigizaji wakubwa Hollywood kama Tom Cruise mwenye $480 million, akiwafuatia na Johny Depp na Tyler Perry ambao wote wana $450 million. srk-tom-johnny 
Listi hiyo imechanganya waigizaji washindi wa tuzo za Academy kama Jack Nicholson ($400 million), Tom Hanks ($390 million) na Clint Eastwood ($370 million) Nicholson ni namba 6 akifuatiwa na Hanks, Bill Cosby, Eastwood na Adam Sandler.

MAMA WA MIAKA 50 AJIFUNGUA KWA NJIA YA KAWAIDA WATOTO WA AJABU HUKO HANDENI-TANGA

Mwajuma Seif-Sio picha yake ya kipindi hiki
Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya upandikizaji.
Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia ya upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.
Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa .
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi.
Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound (kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake.
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza kumsafirisha kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi maalumu hadi siku ya kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.
Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa hakuwa wa kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji na saa moja baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku moja na akafariki.
“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana. Huu ni uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka maji hadi mwili ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea kuishi kwa saa 24,” anasema Dk Mushi.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili, lakini iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa mbali. Hana kiuno wala mikono.

Saturday, May 17, 2014

Wema Sepetu na Aunt Ezekiel Wamwingiza JB Mkenge.

IMEKULA kwake! Wauza nyago kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wamemuingiza mkenge staa mwenzao, kaka mkubwa Jacob Steven ‘JB’ baada kukubali mwaliko kisha kumkatalia dakika za mwisho.

Habari za ndani zilidadavua kwamba JB na wasanii hao walitakiwa kusafiri kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa huko ambapo walipelekwa na uongozi wa Ukumbi wa Princess Cassino uliopo Posta jijini Dar.

Katika hali ya kushangaza, uongozi huo ukiwa tayari umeshawakatia tiketi za daraja la kwanza (first class) zinazogharimu kama dola elfu moja (zaidi ya Sh. milioni 1.6) kila mmoja na baadhi ya wasanii kama Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Wema na Aunt Ezekiel walikataa siku moja kabla ya safari.

Chanzo chetu makini kilipenyeza habari kuwa, Wema na Aunt walichomoa safari hiyo baada ya kuhisi haikuwa na maslahi kwao na walivyopeleka maombi yao ya kimaslahi kwa JB, aliwaambia ni safari ya kujifurahisha na hakuna fedha yoyote watakayopata.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Aunt ambaye alikiri kuchomoa safari hiyo baada ya kushindwana kimaslahi.

“Unajua ile ni kwenda kutangaza biashara ya mtu kwa hiyo sisi tuliwatajia kiasi cha fedha ambacho tulikitaka kulipwa lakini tulishindwana ndiyo maana tukakataa kusafiri maana hatuwezi kufanya kitu ambacho hakina maslahi kwetu na kwenda kuwafaidisha wengine,” alifunguka Aunt.

Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ aliilaani safari hiyo na kusema kwamba JB ni mnafiki kwani aliwachagua wasanii wachache kwa upendeleo ambao baadhi yao wamemwangusha kwa kutokwenda.

“Ukweli nimegundua JB ni mbinafsi, nilikuwa naambiwa lakini nikawa namtetea, sasa nimeamini kwamba hafai akirudi lazima nitamuita, nitazungumza naye kwa nini aliamua kufanya hivyo wakati kila kitu kinapotokea iwe safari au vitu vingine huwa sisi Bongo Movie Unity tunashirikishana lakini kwa hili ameona afanye mwenyewe,” alisema Steve Nyerere.

Jina Kabula Amteka Kimapenzi Madee Wanaongozaja kama Kumbi Kumbi.

Siku za Karibuni Mwigizaji wa Sinema za Kibongo Jina kabula inasemekana amelinasa penzi la Mwaimbaji maarufu wa Bongo Flava Madee .

Habari zilizozagaa ni kuwa huwa jamaa wanaongozana kila mahali kama kumbi kumbi iwe shopping kwenye maduka na hata sehemu za kuogelea...
Baada ya Madee kutafutwa amekana tuhuma hizi na kusema kuna kazi wanafanya pampja ndio maana wanatembea wote kila mahali ...Jina kabula Aliwahi kutoka na Tuesday mwigizaji mwenzake ni walipata mtoto pia siku za karibuni alikuwa anatoka na Bushoke.

Saturday, May 10, 2014

ATHARI:-Wale Warembo……Tazama kile kilichomtokea Dada huyu kwa sababu ya Kutumia Wigi.

Baadhi ya wanawake wengi wa hapa mjini wameanza kutumia style mpya ya kugundisha nywele aka wiving katika vichwa vyao kwa kutumia gundi pasipo kujua mazara yake.

Watafiti na Madaktari kutoka Bara ya Ulaya wamethibitisha kuwa gundi hizo zinazotumiwa huwa zinakemikali ambayo zinaleta adhari kubwa katika mwili wa mwanadamu hususani kansa. 

Mpaka sasa madaktari bingwa kutoka ulimwenguni kote bado hawajapata uvumbuzi wa dawa ya kutibu kansa zaidi tu ya kutumia njia ya kuchomelea mionzi ili mgonjwa apate ahueni.

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar waingia katika mkataba wa kustisha vita.
Wanaume wasio na ajira wako katika hatrari ya kuathirika zaidi kutokana na ugomvi
Ugomvi wa mara kwa mara baina ya wapenzi, marafiki ama hata jamii unaongeza hatari ya kufa kwa watu wenye umri wa makamo.Haya ni kwa mujibu wa watafiti nchini Denmark.
Watafiti wamesema kuwa wanaume na wale ambao hawana kazi wako katika hatari Zaidi.
Utafiti huo katika jarida la 'Epidemiology and Community Health',unasema kuwa shughuli za kukidhi matakwa na mahitaji ya jamii pia zimehusishwa na idadi kubwa ya vifo vya mapema.
Pia kulingana na utafiti huo utu wa mtu na uwezo wa mtu binafsi kukabiliana na dhiki ilichangia katika matokeo ya utafiti huo.
Ingawa watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Copenhagen waliweza kupata uhusiano uliopo kati ya vifo vya mapema na kugombana, na kuwa ugomvi uliongeza hatari ya vifo vya mapema mara tatu, hawakuweza kuelezea kikamilifu sababu haswa ya hali hiyo.
Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa watu wenye wasiwasi mwingi na mahitaji mengi kutoka kwa wapenzi wao na watoto, pamoja na wale wanao gombana mara kwa mara na jamaa wao, wamo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua magonjwa ya moyo na kiharusi.
Tafiti za hapo awali pia zaonyesha kuwa utangamano mwema na watu pamoja na marafiki wengi ina athari chanya katika afya, huku utu kwa kiasi kikubwa ukiamua jinsi mtu hupokea na kuguswa na hali za kijamii pamoja na mahusiano.

Wapendanao hawapaswi kugombana

Kumsumbua mpenzi wako pia kunahatarisha afya
Katika utafiti huu, watafiti walisema kuwa athari za kisaikolojia zinazosababishwa na dhiki, kama vile shinikizo la damu na ongezeko la athari ya magonjwa ya moyo, ndizo hasa zinaweza kueleza athari ya ongezeko la vifo vya mapema.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanapokabiliwa na hali za dhiki kwa kuongeza homoni inayokabiliana na hali ya dhiki na wasiwasi, jambo ambalo linazidisha athari ya kiafya.
Utafiti huo ulihusisha watu 9,875 wake kwa waume wenye umri wa kati ya miaka 36 na 52 na ulitumiwa kuchunguza uhusiano uliopo baina ya hali ngumu ya uhusiano wa kijamii na vifo vya mapema.
Wote walikuwa wameshiriki katika Utafiti ‘Denmark Longitudinal’ kuhusu Ajira, ukosefu wa ajira na afya , kuanzia mwaka wa 2000.
Utafiti uligundua kuwa wasiwasi wa mara kwa mara au mahitaji yanayotokana na wapenzi na watoto ulihusishwa na ongezeko la kufikia 50%- 100% la vifo vya mapema.
Ukosefu wa ajira ulionekana kuongeza athari hasi za uhusiano mgumu wa kijamii. Wale ambao hawako kazini wameonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo kutokana na jambo lolote kinyume na wale walio na kazi.
wanaume pia wako katika hatari zaidi kutokana na mahitaji na wasiwasi unaotokana na wapenzi wao wa kike , huku wakiwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo zaidi ya ile ambayo kwa kawaida imehusishwa na kuwa mwanamume.
Dakta Rikke Lund, wa kitengo cha afya ya u,mma katika chuo kikuu cha Copenhagen amesema kuwa wasiwasi na ugomvi ni sehemu ya maisha. Lakini akaongeza kuwa watu ambao wanakuwa na migogoro mara kwa mara wako katika hatari zaidi lakini wanaweza wakasaidiwa.

WATCH P SQUER NEW VIDEO I MEAN TEST MONEY
alone but happy

Video ya Taste the Money ya P.Square imetoka.Itazame Hapa.

P-Square-Taste-The-Money-Art2P.Square ni miongoni mwa wasanii wachache kutoka Afrika ambao wamekua na bahati kubwa ya baadhi ya nyimbo zao zinapotoka kuhit kwa haraka,Taste the Money audio ilitoka February 11 na kuwa ni mojawapo ya hit iliyoshika kwa haraka,hii hapa video yao icheki imeongozwa na Jude Engees Okoye.

Ufuska Bongo Movies Wamkosesha Deal Mwigizaji Nora.

MWANADADA wa ‘long time’ kwenye sanaa ya uigizaji amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukosa dili za kazi za maana kutokana na tabia za kifuska kwa baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo Movie.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nora alisema amekuwa akitembelea katika ofi si mbalimbali
na kila anapojitambulisha kwamba ni msanii wa fi lamu watu wanashtuka na sehemu nyingine anakosa dili za maana kutokana na uchafu wa baadhi ya wasanii hasa wasagaji na wanaojiuza.

“Yaani naona aibu sana kujitambulisha kwenye ofi si za watu kwani kila ninakoenda na kujitambulisha watu wanaanza kunong’ona huku wakidai kwamba wasanii wa kike wa fi lamu wana tabia chafu wakati tunachafuliwana watu wachache tu wasiojiheshimu,” alisema Nora.
 

Maimartha Atuhumiwa Kuwauzia Mastaa Dawa za Kukuza Makalio

MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za moto kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.

“Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.

“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa,”  alisema sosi huyo.

Akaongeza: “Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu)   ndiye aliyemsababishia kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa hizo.”

Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila kugundulika.

Mai akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa ya habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama ni vidonge au losheni.”

Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake linauza urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.

“Kama nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka langu linadili na urembo wa aina zote,” alisema Mai akishindwa kufafanua zaidi.

Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa za Mai alisema: “Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya kuongeza makalio.

Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.”
Stori: : Hamida Hassan na Gladness Mallya, GPL

Lupita Akiwa Na Rais Obama Na Mke Wake Michelle Obama Ndani Ya White House.

LL 7
 Amefuatilia na vyombo vingi vya habari duniani toka alivyofanya filamu ya 12 Years A Slave na kupata tuzo ya Oscar. 

Lupita ameandikwa na magazeti na majarida makubwa kuhusu mambo tofauti kama filamu, familia na mitindo ya mavazi. 

Hivi karibuni alipata mwaliko wa kwenda White kuonana na Obama pamoja na watu tofauti kwenye  chakula cha usiku.
l 2Lupita-na-Obama-1 Lupita-na-Obama-2


Kutana na Huyu Star Wa Hollywood anayekula Udongo.

 ?????????????????????
 Muigizaji maarufu wa Hollywood nchini Marekani, Shailene Woodley,amesema wiki hii kuwa  yeye hupenda kula udongo kila siku ili kuwa na afya bora. 

Shailene anasema hupima kijiko kimoja cha udongo na kula kila siku.
Shailene alinukuliwa akisema kuwa “Udongo unampa afya bora mwilini na anaonekana kama chizi akisema hivyo ila anaamini ni kweli, udongo unasafisha mwili na kukuweka sawa muda wote”
sss 2
Tabia hii alijifua kutoka kwa dereva mwafrika na aliona wakisafisha udongo kabla ya kitendo cha kuula. 

Wanasayanci wanameipa jina tabia ya kula udongo kuitwa Geophagy.

Wednesday, May 7, 2014

Baada ya Ferguson – Rio Ferdinand nae anakuja na kitabu chake

article-2621486-1BDADBAE000005DC-542_634x470 
Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akizua mijadala mingi kwenye vyombo vya habari kutokana na vitu alivyoandika kwenye kitabu chake.

 Hivi sasa beki Rio Ferdinand ambaye anakaribia kuondoka ndani ya klabu ya Man United nae anajiandaa kutoa kitabu chake ambacho kinatajwa kitafunua yote ya nyuma ya pazia kuhusu utawala wa David Moyes.
Ferdinand, 35, anatarajiwa kuandika yote yanayohusiana na maisha yake ya soka kwenye kitabu ambacho kitapewa jina la ‘#2sides: Rio Ferdinand – My Autobiography.’
Kitabu chake kinatarajiwa kueleza kiundani msimu mbovu kuliko yote ndani ya klabu hiyo kufuatia kuondoka kwa kocha Alex Ferguson na timu kukabidhiwa kwa David Moyes ambaye alitimuliwa wiki kadhaa zilizopita – huku wachezaji wakubwa kama Ferdinand wakitajwa kuwa na mkono kwenye kutia mchanga kibarua cha Moyes.
Kitabu hicho kinatarajiwa kutoka October 2 na kinachapishwa na kampuni ya Blink Publishing

Nikki wa Pili Na Ujio Mwingine Mpya.

Nikki wa II - Staki KaziMshindi wa tuzo ya wimbo bora wa Hip hop Nikki wa pili leo ametoa cover ambayo inamaanisha ujio wake mwingine unaofuata baada ya Nje ya box ambayo ilitoka siku ya Valentine February 14 2013,ingawa katikati kuna single kadhaa zimetoka kwa kundi kama Weusi ambao nao ndiyo wameibuka na ushindi wa kundi bora 2013/2014.

Wimbo unaitwa Sitaki kazi haijafahamika bado kilichoimbwa ndani ni nini ila kilichoelekezwa ni tarehe rasmi ya kuachiwa kwa wimbo huo ambao itakua ni Mei 13 na imetengenezwa na producer yule yule wa Nje ya box,bei ya mkaa na baadhi ya hits za Weusi,ndani humu kawakutanisha Ben Pol na G nako.

Saturday, April 12, 2014

VIJANA WAUZA JINA LA TANZANIA DUNIAN
Timu ya watoto wa Tanzania iliyonyakua kombe la dunia
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya nchi hiyo kwa kutwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Tanzania imesema Rais Kikwete afurahishwa jinsi watoto hao walivyonyakua kombe hilo la dunia.
"Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana" Rais amesema.
Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ilipangwa kundi la 2 ambapo pia zilikuwapo timu kutoka Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi.
Makundi yaliyopangwa yalikuwa matatu.
Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kumenyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwenye fainali kwa mabao 3-1.
"
Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi". Rais amesema na kuwaasa watoto "ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya" Ameongeza Rais Kikwete .

Friday, April 11, 2014

MECHI ZA LEO

Premier League View all fixtures
3:07 PM
Crystal Palace FC Crystal Palace
v
Aston Villa FC Aston Villa
ODDS
3:07 PM
Fulham FC Fulham
v
Norwich City FC Norwich City
ODDS
3:07 PM
Southampton FC Southampton
v
Cardiff City FC Cardiff City
ODDS
3:07 PM
Stoke City FC Stoke City
v
Newcastle United FC Newcastle United
ODDS
3:07 PM
Sunderland AFC Sunderland
v
Everton FC Everton
ODDS
3:07 PM
West Bromwich Albion FC West Bromwich Albion
v
Tottenham Hotspur FC Tottenham Hotspur
ODDS
Primera División View all fixtures
3:00 PM
Real Club Celta de Vigo Celta de Vigo
v
Real Sociedad de Fútbol Real Sociedad
ODDS
5:00 PM
Villarreal Club de Fútbol Villarreal
v
Levante UD Levante
ODDS
7:00 PM
Granada CF Granada
v
FC Barcelona Barcelona
ODDS
9:00 PM
Real Madrid Club de Fútbol Real Madrid
v
UD Almería Almería
ODDS
FA Cup View all fixtures
5:07 PM
Wigan Athletic FC Wigan Athletic
v
Arsenal FC Arsenal
ODDS
Bundesliga View all fixtures
2:30 PM
Borussia VfL Mönchengladbach Borussia M'gladbach
v
VfB Stuttgart 1893 Stuttgart
ODDS
2:30 PM
SC Freiburg Freiburg
v
Braunschweiger TSV Eintracht 1895 Eintracht Braunschweig
ODDS
2:30 PM
Hannover 96 Hannover 96
v
Hamburger SV Hamburger SV
ODDS
2:30 PM
1. FSV Mainz 05 Mainz 05
v
SV Werder Bremen Werder Bremen
ODDS
2:30 PM
VfL Wolfsburg Wolfsburg
v
1. FC Nürnberg Nürnberg
ODDS
5:30 PM
FC Bayern München Bayern München
v
BV Borussia 09 Dortmund Borussia Dortmund
ODDS
Serie A View all fixtures
5:00 PM
US Sassuolo Calcio Sassuolo
v
Cagliari Calcio Cagliari
ODDS
7:45 PM
AS Roma Roma
v
Atalanta Bergamasca Calcio Atalanta
ODDS
Ligue 1 View all fixtures
4:00 PM
Lille OSC Métropole Lille
v
Valenciennes FC Valenciennes
ODDS
7:00 PM
AC Ajaccio Ajaccio
v
FC Girondins de Bordeaux Bordeaux
ODDS
7:00 PM
Evian Thonon Gaillard FC Evian TG
v
SC Bastia Bastia
ODDS
7:00 PM
OGC de Nice Côte d'Azur Nice
v
FC Lorient-Bretagne Sud Lorient
ODDS
7:00 PM
Stade Rennais FC Rennes
v
AS Monaco FC Monaco
ODDS
7:00 PM
FC Sochaux-Montbéliard Sochaux
v
Toulouse FC Toulouse
ODDS
Eredivisie View all fixtures
5:45 PM
Go Ahead Eagles Go Ahead Eagles
v
SC Heerenveen Heerenveen
ODDS
6:45 PM
SC Cambuur Leeuwarden Cambuur
v
SBV Vitesse Vitesse
ODDS
7:45 PM
FC Twente Twente
v
SV Roda JC Roda JC
ODDS
All kick-off times stated as BST