Jokate Mwegelo aeleza anachokipenda na asichokipenda kwa wasichana wa Tanzania.

Kama mrimbwende amewasifia wasichana wa Tanzania kwa jinsi wanavyojua kuweka sawa na kupendeza.
“kitu
ambacho nakipenda, napenda kwa sababu wanapendeza, wanapenda
like..kupendeza, wanajitunza vizuri.” Jokate amefunguka kupitia The
Switch ya 100.5 Times Fm.
Lakini kwa upande wa kile ambacho anaona hakiko sawa, uvivu ndio anaoupigia mstari.
“Kitu ambacho sikipendi, ni kwamba…yaani sijui niseme kwamba hawajitumi sanaa. Yaani bado sijaona njaa ile.” Amesema Jokate.
“Kwa
mfano ukiangalia kwa mfano Marekani sasa hivi, all top artists ni
wasichana, kwa hiyo females wanahustle. Wasichana wakibongo tumezoea
sijui kupewapewa au kutafuta kupitia njia za kimkatomkato. That’s a
thing ambacho mimi sikipendi na sitakiappreciate maisha yangu yote.”
Amefunguka Kidoti.
Amefunguka
kuwa wasichana wana fursa nyingi zaidi ya wanaume na kwa kuwa wamepewa
akili pia ni vyema wakazitumia kwa kiwango kinachotosha, “make the most
of it.”
Lakini
pia amekubali kuwa kuna wasichana wengi pia ambao wanaofanya vizuri ,
wasomi na wanaoweza kujituma na wanaongoza katika nyanja mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS