urday, March 01, 2014

Mshambuliaji wa Chelese, Samuel Eto’o amechukizwa na kauli iliyotolewa na kocha wake Jose Mounrinho, kauli iliyoonekana kukeje umri wa mshambuliaji huyo kuwa sehemu ya kikwazo cha timu yake kupata ushindi dhidi ya Galatasaray.
Kipande
cha video kinachoonesha maongezi ya Mourinho kilirushwa na Canal Plus,
ambapo ilikuwa ni sehemu ya maongezi faragha kati yake na mfanyabiashara
mmoja.
“Tatizo la Chelsea ni kwamba nakosa mfungaji. Eto’o ana miaka 32, labda 35, nani anajua?” alisema Mounrinho.
Hata
hivyo Samuel Eto’o ambaye ana umri wa miaka 32, alijibu pia kwa kejeli
kwa kutumia takwimu ile ile aliyoitoa Mourinho, na kudai kuwa kama
aliweza kufunga magoli matatu dhidi ya Manchester akiwa na miaka 37 basi
anaweza kufunga magoli mengi zaidi hata akiwa na miaka 50.
Baada
ya maelezo ya Mourinho kuoneshwa kwenye television, kocha huyo aliomba
radhi na kueleza kuwa bado uhusiano wake na Eto’o haukuathiriwa na tukio
hilo.
Naye
Caude Le Roy aliyewahi kufanya kazi na timu ya taifa ya Cameroon
alieleza kuwa aliongea na Eto’o kwa njia ya simu na kwamba alionesha
kukasirishwa na kauli ya Mourinho.
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS