turday, March 01, 2014

Msanii
wa filamu za Kiswahili, Aunt Ezekiel ambaye anatarajia kuachia wimbo
wake mpya wa Bongo Flava alioupa jina la ‘Mguu kwa Mguu’
aliomshirikisha Linex Mjeda, ameeleza sababu kubwa iliyomfanya aingie kwenye game la Bongo Flava.
“Unajua
game la Tanzania linabadilika badilika kwa hiyo nimeona ngoja pia
nijihusishe katika uimbaji ili niendelee kuteka mashabiki, mimi zamani
nilikuwa napenda sana Bongo Flava na sio kwamba nilikuwa naimba hapana,
nilikuwa kama nikiona wasanii wakianza kuimba basi moyoni nafurahi sana.
Siku moja wakanipa ushauri na hapo ndipo nikaingia studio na
kutengeneza wimbo wa ‘Mguu kwa Mguu.” Aunt Ezekiel ameiambia tovuti ya
Times Fm.
Ameeleza kuwa alitegemea kuachia wimbo huo mwaka jana ila ratiba zake hazikwenda vizuri hivyo aliamua kuiachia rasmi mwaka huu.
Mguu kwa Mguu ni wimbo uliotayarishwa na Mr. T Touch ndani ya Seductive Records .
No comments:
Post a Comment
ADD COMMENTS