Translate

Friday, February 28, 2014

TAARIFA KUHUSU KUACHISHWA KAZI KWA KOCHA WA TAIFA STARS

Thursday, February 27, 2014

TAARIFA KUHUSU KUACHISHWA KAZI KWA KOCHA WA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

Tuesday, February 11, 2014

Linex akanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na Agnes Masogange, 'Sina haraka ya kuwa na mpenzi'

Tuesday, February 11, 2014

Linex akanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na Agnes Masogange, 'Sina haraka ya kuwa na mpenzi'

Kupitia akaunti yake ya Facebook, mkali huyo wa ‘Kimugina’ ameonesha kusikitishwa na habari iliyoandikwa na tovuti moja kuwa yeye na Agnes wako kwenye mapenzi mazito.
“ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Ameandika kwenye Facebook.
Wikendi hii, Linex alipost picha mbili Instagram akiwa na mrembo huyo, moja wakiwa wamepoz ufukweni, na nyingine akiwa naye katika mechi ya mpira wa kikapu kati ya timu za madirector wa video za muziki Tanzania, Adam Juma na Karaban.